Umoja wa Mataifa juzi umetoa orodha ya mataifa yenye furaha zaidi duniani. Finland kwa mara nyingine tena imeibuka nafasi ya kwanza, kutokana na huduma bora wananchi wa taifa hilo wanapata kutoka kwa serikali. Kenya iko katika nafasi ya 114 duniani. Sepetuko inakiri kuwa Wakenya wengi hawana furaha kutokana na ugumu wanaopitia, huku serikali ya siku ikionekana kutojali. Wakenya watafurahi vipi wakati madaktari wanaendelea na mgomo, nafasi za ajira hazipo nchini, ufisadi umesheni serikalini, fedha za kufadhili elimu zinacheleweshwa miongoni mwa masaibu mengine.