Katika msururu wa leo wa kipindi cha Kulikoni, Prof Monda anaongea na Bwana Charles Masawe, mkurugenzi mkuu wa shirika lisilo la serikali la Simba's Footprints Foundation ambalo lipo Moshi Tanzania. Shirika hili linachangia maswala mengi ya jamii, elimu kwa watoto wa mitaani na miradi ya maji na elimu Tanzania. Pia, wanashirikiana na shirika zingine za kutoka Kenya kuendeleza mchango wa wanadiaspora katika shuguli za Afrika Mashariki kupitia sanaa na mziki. Karibu kwenye kipindi!