Silas Githaiga, mkazi wa Kijii cha Giciria, Kaunti ya Nyeri alikuwa mraibu wa mihadarati kwa miaka takriban 14. Anasema uraibu huo ulilemaza masomo yake na akiwa katika shule ya upili alisomea shule nne tofauti kwa vile alikuwa akifukuzwa kutokana na utovu wa nidhamu. Anasema tatizo hilo liliathiri ndoa yake likazima ndoto ya kuwa mhadhiri wa chuo kikuu na hata safari yake ya kwenda ughaibuni. Hata hivyo aliamua kurekebisha na hapo ndipo alipojiunga na chuo cha urekebishaji tabia. Kwa sasa maisha yake yamebadilika na ameamua kuwa mstari wa mbele kuwahamasisha vijana dhidi ya utumiaji wa dawa za kulevya vilevile kuwapa ushauri nasaha. Pata masimulizi kamili katika Kisa Changu Podcast na Edwin Mbugua.