Hatua ya Kiongozi wa Kanisa la Kianglikana, Jackson Ole Sapit kuwanyima fursa wanasiasa kuhutubu katika mimbari kwenye halfa aliyokuwa akiongoza katika Eneo Bunge la Butere, Kaunti ya Kakamega, imeendelea kuibua mijadala mikali. Je, ndio mwisho wa maendeleo na ujenzi wa makanisa baada ya wanasiasa kunyimwa fursa ya kuzungumza mimbarini? Mwanahabari wetu Victor Mulama amemhoji Askofu wa Kanisa Katoliki Dayosisi ya Nyeri Anthony Muheria ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Madhehebu la Kushughulikia Kanuni za Kuzingatiwa katika Maeneo ya Ibada.