SIASA PODCAST: Mbona Raila anaogopwa Mlima Kenya? Wazee Wazungumza
Published Jul. 31, 2021
00:00
00:00

Tangu Kenya ipate uhuru, jamii za Luo na Agikuyu zimekuwa na uhasama mkali wa kisiasa na hata kwa wakati mmoja Rais wa kwanza Mzee Jomo Kenyatta akamweka kizuizini Jaramogi Oginga Odinga. Naye Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga wamekuwa na makabiliano makali ya kisiasa hasa wakati wa kampeni kabla ya handshake. Lakini je, uhasama huu ulianzia wapi? Mwanahabari wetu John Mbuthia amezungumza na wazee wa jamii ya Agikuyu kuhusu suala hili wakijibu maswali ya chimbuko la uhasama baina ya jamii hizi mbili, kuendelezwa kwa uhasama huu kati ya Raila na Uhuru Kenyatta vilevile ushirikiano wa viongozi hawa wawili mbinu ikiwa kumkaribisha Raila kwenye eneo la Kati kutumia wafanyabiashara na wasanii wa Mlima Kenya.