Katika sehemu hii ya kwanza tutaangazia, aina ya megu za nazi , jinsi ya kuandaa mbegu za mnazi, upanzi wake vilevile utunzaji wa mnazi pale shambani hadi kuvuna bidhaa mbalimbali za mnazi zikiwamo madafu, nazi, Makuti, vifuvu vya nazi na kadhalika. Pia tutaangazia aina ya mchanga ambao mnazi hufanya vizuri zaidi, kumbuka ipo dhana kwamba mnazi hufanya vizuri katika Eneo la Pwani pekee. Nimemshirikisha mtaalamu vilevile mkulima wa Mnazi katika Eneo la Pwani Bwana Emmanuel Masha kutoka Eneo la Palakumi, katika Eneo Bunge la Ganze Kaunti ya Kilifi.