Huduma za Afya Zimepooza kwa Siku 40: Serikali Inawajali Wakenya Kweli?
Sepetuko
Apr. 24, 2024
Kwa zaidi ya siku 40, Wakenya wameendelea kukosa huduma za matibabu katika hospitali za umma kufuatia mgomo wa madaktari. Madai ya serikali eti kunao mwafaka unaoelekea kutiwa saini kati yake na madaktari inaonekana ilikuwa njama tu ya kuwashinikiza madaktari kusalimu amri. Hii ni serikali aina gani inayowachezea watu wake kiasi hiki? Mbona idai kuna mwafaka ilhali huo sio ukweli? Nani anamjali Mkenya wa kawaida?
RELATED EPISODES
Matukio ndani ya UDA yanaonyesha upungufu wa sera.
Bunge la Kitaifa Laanza Msasa wa Mawaziri Walioteuliwa