Kisa Changu Podcast: Nina sehemu mbili za siri; wanawake wakanidhulumu
Kisa Changu
Jul. 02, 2022
Beatrice Wawera mwenye umri wa miaka 24 amekuwa katika njiapanda tangu utotoni hadi sasa. Anasema alipokuwa mdogo hakujua alikuwa tofauti na wasichana wengine kwani alizaliwa na sehemu mbili za siri - ya kiume na kike na wazazi wake walimtambua kuwa msichana. Lakini alipoanza kubaleghe, mambo yalianza kubadilika. Anasema hakuwa na matiti wala kupata hedhi kama wasichana wengine. Isitoshe, alianza kupata hisia za kimapenzi kwa wasichana wengine hali iliyomchanganya hata zaidi hasa baada ya kudhulumiwa na wasichana ao, hao. Anasema maisha hayajakuwa rahisi na hata wakati mmoja alijaribu kujiua. Je, imekua vipi na safari yake ya kujitambua rasmi kuwa mwanaume imefikia wapi? Fahamu zaidi katika makala haya ya Kisa Changu Podcast na Carren Omae.
RELATED EPISODES
Eliot Berry, Mwingereza anayependelea kuishi Kenya| Kisa Changu Podcast
Familia zatafuta wapendwa wao, Kilifi | Kisa Changu Podcast