Kisa Changu Podcast: Kilio cha Mama
Kisa Changu
Apr. 09, 2022
Ruth Keino mkazi wa Nandi ni mama mwenye machungu. Keino amekuwa akitafuta haki tangu mwanawe alipoaga dunia zaidi ya mwaka mmoja uliopita akiwa shuleni. Beryl Cherop aliyekuwa na miaka 16 alifariki dunia miezi michache tu baada ya kujiunga na kidato cha kwanza katika Shule ya Upili ya St Teresa of Avila Girls. Kinachomuumiza Keino roho hata zaidi ni kwamba hakuna mtu ahta mmoja aliyehudhuria hafla ya mazishi ya mwanawe kuifariji familia. Anasema hatachoka hadi pale haki itakapopatikana kufuatia kifo cha mwanawe. Sikiliza masimulizi ya kina katika makala yafuatayo
RELATED EPISODES
Eliot Berry, Mwingereza anayependelea kuishi Kenya| Kisa Changu Podcast
Familia zatafuta wapendwa wao, Kilifi | Kisa Changu Podcast