Kisa Changu Podcast; Kwa nini niliamua kuwasaidia wanaougua fistula - Sharon Korir. Sehemu ya 2
Kisa Changu
Jan. 30, 2022
Katika sehemu ya pili Wakili Korir anaeleza namna mahangaiko yake yalivyompa msukumo wa kuanzisha Shirika la Save a Woman, Fistula Foundation ili kuwapa matumaini wanawake na wasichana ambao wameathiriwa na Fistula. Akiwa wakili kwa ushirikiano na washikadau mbalimbali, anahisi serikali haijafanya vyema sana katika kuihamasisha jamii kuhusu Fistula hali ambayo imechangia kuwapo kwa unyanyapaa dhidi ya wanawake wanaougua Fistula. Sikiliza masimulizi haya katika sehemu hii ya pili na Carren Papai.
RELATED EPISODES
Eliot Berry, Mwingereza anayependelea kuishi Kenya| Kisa Changu Podcast
Familia zatafuta wapendwa wao, Kilifi | Kisa Changu Podcast