Gumzo la Wiki Podcast: Raila debeni 2022; Wana'OKA watamuunga nani?
Siasa na Gumzo
Dec. 12, 2021
Tangazo la Odinga kuwania urais kwa mara ya tano, ni ithibati kamili kwamba kinyang'anyiro kitakuwa kati yake na William Ruto. Je, hatima ya Kalonzo, Mudavadi na Wetangula ambao walikosa kufika Kasarani ni ipi? Aidha, Wakfu wa Mlima Kenya Foundation, MKFumesema Raila tosha. Je, unadhani wafanyabiashara hao wataamua mwelekeo wa siasa za Mlima Kenya ama ni wananchi ndio watakaoamua jinsi anavyosisitiza William Ruto? Wanahabari wetu, John Mbuthia wa Nyeri, Moses Kiraise wa Pokot Magharibi na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wameshiriki gumzo na wakazi wa maeneo yao.
RELATED EPISODES
Kujiunga kwa ODM Na Serikali Kutakomesha Maandamano ya Gen Zs?
Hasla Akosa Usingizi Kufuatia Gharama ya Maisha | Siasa na Gumzo Podcast
Uteuzi wa Makatibu Wazua Tumbojoto, Raila akitaka Waluke Kuachiliwa | Siasa na Gumzo Podcast