SIASA PODCAST: Mbona Raila anaogopwa Mlima Kenya? Wazee Wazungumza
Siasa
Jul. 31, 2021
Tangu Kenya ipate uhuru, jamii za Luo na Agikuyu zimekuwa na uhasama mkali wa kisiasa na hata kwa wakati mmoja Rais wa kwanza Mzee Jomo Kenyatta akamweka kizuizini Jaramogi Oginga Odinga. Naye Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga wamekuwa na makabiliano makali ya kisiasa hasa wakati wa kampeni kabla ya handshake. Lakini je, uhasama huu ulianzia wapi? Mwanahabari wetu John Mbuthia amezungumza na wazee wa jamii ya Agikuyu kuhusu suala hili wakijibu maswali ya chimbuko la uhasama baina ya jamii hizi mbili, kuendelezwa kwa uhasama huu kati ya Raila na Uhuru Kenyatta vilevile ushirikiano wa viongozi hawa wawili mbinu ikiwa kumkaribisha Raila kwenye eneo la Kati kutumia wafanyabiashara na wasanii wa Mlima Kenya.
RELATED EPISODES
Hali ya siasa Afrika Mashariki na mizozo ya DRC na Sudan: Kulikoni Podcast
Je, hanshake ingine ndio suluhu la Kenya?
Nilikuwa darasa moja na Dr. Ruto, Rais Mteule
Daily Brief Podcast; Is Uhuru learning from DP Ruto? Episode 1